“Lima Platform” ni jukwaa la usimamizi na kujifunza maarifa mbalimbali ya shamba kwa lugha ya Kiswahili linalowawezesha wakulima vijana wenye umri wa miaka 15 – 35 kupata maarifa na ujuzi kuendesha kilimo katika ulimwengu wa kidijitali. Jukwaa hili linatoa mafunzo, mwongozo wa kilimo bora, na mbinu za kisasa za kilimo kupitia teknolojia ya kisasa. Lima Platform inawalenga vijana ambao wanataka kujifunza na kuboresha ujuzi wao katika sekta ya kilimo, na inawapa fursa ya kuunganishwa na wataalamu wa kilimo, kushiriki uzoefu na maarifa, na kupata taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia kuboresha uzalishaji wao na kuongeza kipato.
Dira yetu ni kuwawezesha vijana wakulima katika Afrika Mashariki na Kati kupata maarifa na ujuzi wa kisasa wa kilimo ili kuongeza tija na kipato chao kwa kutumia teknolojia za kidijitali.
Lengo letu ni kuwaweka vijana wakulima mstari wa mbele katika matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kilimo, kuhakikisha wanapata taarifa sahihi na zana bora za usimamizi wa mashamba yao.