Papai huitwa ‘mfalme’ wa matunda mengine kwasababu limesheheni kila aina ya vitamini, zikiwamo A, B, C, D, E na K pia kuna potassium na magnessium na copper. Hivyo ni muhimu kua na utamaduni wa kula papai kwa wingi. Zijue faida kemkemkupitia na upone sasa
- Tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye papai husaidia katika kuzuia kupata saratani.
- Wataalamu wa lishe wanasema watu wenye matatizo ya kuugua majipu, uvimbe na vidonda mara kwa mara, huwa na upungufu wa virutubisho muhimu, ambavyo huweza kupatikana ndani ya papai. Watu wenye matatizo hayo wakitumia papai hupata nafuu na kupona haraka.
- Papai huelezwa na wataalamu kuwa husaidia kuleta nuru ya macho, kama inavyoaminika kwa karoti, na tunda hili husaidia pia kupunguza madhara yatokanayo na moshi wa sigara.Kutoka na faida hizo, ni vema wavutaji wa sigara wakatumia tunda hili mara kwa mara.
- Papai linatambulika kwa kuwa na uwezo wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeheka kwa haraka. Ndani ya papai kuna Zeaxanthin hii ni anti-oxidant ambayo inakazi ya kuchuja miale hatari ya jua. Pa inaaminika kuwa antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.
- Vilevile papai huaminika kusaidia kupunguza hatari ya kuwa na ugonjwa wa pumu. Ndani ya papai kuna virutubisho vingi, lakini uwepo wa beta-carotene ndani ya papai husaidia kwa wagonjwa wenye pumu.
- Antioxidanti zilizopo kwenye papai mfano beta-carotene husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya saratani kwa wanaume. Ulaji wa tunda hili husaidia katika kudhibiti upatikanaji wa saratani ya kwenye via vya uzazi hasa saratani ya korodani.
- Vitamini K iliyopo kwenye Papai ni muhimu katika afya ya mifupa. Hivyo ulaji wa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya mifupa na kudhibiti kupasuka kwa mifupa. Vitamin k vilevile husaidia katika ufyonzwaji wa madini ya calcium na huzuia upotevu wa madini haya kupitia mkojo.
- Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa papai pia husaidia wenye kisukari. Tunda hili lipo katika kundi la vyakula vyenye maji kwa wingi. Tafiti zinaonesha kuwa watu wenye kisukari type 1 diabetes wameweza kupunguza kiwango cha sukari mwilini mwao. Wakati huohuo watu wenye kisukari type 2 diabetes wameweza kuimarisha kiwango cha sukari mwilini pamoja na kiwango cha homoni ya insulin.
- Paipai pia lina enzyme zinazoitwa papain hizi husaidia katika mmeng’enyo wa chakula. Pia kama tulivyo sema papai lina maji nmengi na kambakamba vyote kwa pamoja husaidia katika upatikanaji wa choo na kusaidia katika kudhibiti mmeng’enyo wa chakula
- Madini ya potassium (aina ya chumvi) na vitamini vilivyomo kwenye papai husaidia katika kulinda afya ya moyo dhidi ya maradhi hatari yanayoshambulia mfumo wa usukumwaji wa damu mwilini. Ulaji wa madini haya huku ukipunguza ulaji wa madini ya sodium (chumvi hii tunayotumia) husaidia katika kuulinda moyo dhidi ya maradhi hatari kama shambulio la moyo, presha na kiharusi (stroke).
- Katika papai kuna chembechembe ya Choline, haya ni muhimu katika kusaidia miili yetu hasa kulala, kujongea kwa misuli (kukunja na kukunjuka, kutanuka na kusinjaa). Vilevile husaidia katika kulinda mpangilio wa utando wa seli, husaidia katika kutunza kumbukumbu pamoja na kujifunza yaani kusoma. Pia husaidia katika ufyonzwaji wa fati (mafuta).
- Kwa ufupi tunda hili lina matumizi mengi sana kama ukuaji wa nywele na kuzifanya zing’ae, kupona kwa vidonda, ukuaji wa tishu na ukuaji wa mwili kwa ujumla. Na haya yote ni kutokana na kuwepo kwa wingi vitamin C na vitamin A.
Matunda ni dawa. Ni vyema kujitahidi kula matunda na mboga za majani mara kwa mara.
Makala yameandikwa na Lightness Mlay, Mtaalamu wa Lishe, Tanzania.
Je, wewe ni mtaalamu wa Kilimo au Lishe na ungetamani kufanya kazi na jukwaa hili. Tafadhali, wasiliana nasi kupitia info@limaplatform.co.tz au WhatsApp: 0659215984